WATUMISHI WIZARA YA FEDHA WAAGIZWA KUENDELEA KUHUDUMIA WANANCHI SABASABA.

WATUMISHI WIZARA YA FEDHA WAAGIZWA KUENDELEA KUHUDUMIA WANANCHI SABASABA.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua, akitembelea Banda la Wizara ya Fedha ili kuona namna watumishi wa Wizara hiyo na Taasisi zake wanavyotoa huduma kwa wananchi wanaotembelea Banda hilo wakati wa Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua, akizungumza wakati akitembelea watumishi kuona wanavyotekeleza majukumu yao katika Banda la Wizara ya Fedha, alipowatembelea wakati wa Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua (kulia), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo (TIB), Bw. Deogratius Kwiyukwa, baada ya kutembelea Banda la benki hiyo lililopo ndani y…