WATALII WASHUHUDIA MWENGE WA UHURU UKIMULIKA MAAJABU YA NGORONGORO.

WATALII WASHUHUDIA MWENGE WA UHURU UKIMULIKA MAAJABU YA NGORONGORO.
Na Kassim Nyaki, Ngorongoro. Mbio za Mwenge wa Uhuru jana tarehe 6 Julai, 2026 zilliwasili Wilaya ya Ngorongoro na kukimbizwa umbali wa kilomita 386 kuzindua miradi mbalimbali ambapo pia umepita katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro na kuangazia maajabu saba ya Ngorongoro huku watalii kutoka mataifa mbalimbali wakishuhudia. Ukiwa katika hifadhi ya Ngorongoro kuelekea Wilaya ya Karatu watalii kutoka mataifa mbalimbali walionyesha bashasha kuona Mwenge ukipita eneo la hifadhi lenye vivutio mbalimbali ambapo tukio hilo linaashiria uwepo wa Amani, umoja na mshikamano wa Kitaifa unaotoa tumaini kwa wageni kufanya shughuli za utalii bila changamoto yoyote. Mmoja wa wageni kutoka nchini Denmark Ella Wiliams ameeleza kuwa “Tumefurahi kuona Mwenge wa Uhuru ukipita eneo la hifadhi kwa hali ya utulivu na sisi kuwa sehemu ya tukio hili, hii inaashiria kuwa Tanzania pamoja na kuwa na maajabu mengi ya vivutio vya utalii, ni nchi pia yenye amani, umoja na mshkamano unaoshiria Taifa moja lenye watu wanao…