WASHINDI ‘VIJANA UCHUMI CHALLENGE’ WAKABIDHIWA MAMILIONI, SERIKALI KUJA NA MPANGO MAALUM WA MIKOPO KWA VIJANA
WASHINDI ‘VIJANA UCHUMI CHALLENGE’ WAKABIDHIWA MAMILIONI, SERIKALI KUJA NA MPANGO MAALUM WA MIKOPO KWA VIJANA
KATIKA kuhakikisha vijana wanawekwa viti vya mbele katika ajenda ya uchumi Serikali inaandaa maboresho ya kisera na kisheria yatakayowaondolea vijana wajasiriamali kikwazo cha muda mrefu cha ukosefu wa dhamana za mikopo kwa kuimarisha mfumo wa udhamini wa mikopo na kuruhusu matumizi ya dhamana zinazohamishika. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Rais wa Serikali ya Jamuhuri Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya kuwatambua na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la ‘Vijana Uchumi Challenge’ Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema; Serikali inatambua kundi la vijana na kuwepo kwa Wizara maalum inayoshughulikia masuala ya vijana ni moja ya mkakati wa kuhakikisha kuelekea uchumi endelevu vijana wanakuwa sehemu ya mafanikio hayo kupitia mawazo na ubunifu yenye kutatua changamoto za kijamii na uchumi. Amesema; Serikali inaandaa maboresho ya kisera na kisheria yatakayowaondolea vijana wajasiriamali kikwazo cha muda mrefu cha ukosefu wa dhamana…