Washindi Tuzo ya Kiswahili ya Safal kujulikana Ijumaa
Washindi Tuzo ya Kiswahili ya Safal kujulikana Ijumaa
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa ALAF Limited, Hawa Bayumi (katikati) akitangaza orodha fupi ya waandishi waliofanikiwa kutinga fainali ya Tuzo ya Kiswahili ya Safal ya Fasihi ya Afrika 2025. Wengine kutoka kushoto ni Afisa Huduma kwa Wateja Tito Maliyalabu, Meneja Msaidizi wa kitengo cha Rasilimali watu Nyamizi Malatu, Meneja Mauzo ya Miradi, Tom Mwita na Afisa Uhusiano kwa Wateja, Grace Gabriel. TUZO ya Kiswahili ya Safal ya Fasihi ya Afrika imetangaza orodha fupi ya miswada saba katika vipengele vitatu — riwaya, ushairi, na makusanyo ya hadithi fupi — ikiwa ni utangulizi wa hafla ya utoaji tuzo hizo kwa msimu wa 10, inayotarajiwa kufanyika Julai 24, mwaka huu, jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo inadhaminiwa na kampuni ya Safal Group, kupitia kampuni zake tanzu za Mabati Rolling Mills ya Kenya na ALAF iliyoko nchini Tanzania. Tuzo ya Kiswahili ya Safal ya Fasihi ya Afrika ilianzishwa mwaka 2014 na Dkt. Lizzy Attree na Dkt. Mukoma wa Ngũgĩ ili kutambua kazi za uandishi katika…