WANANCHI WAPONGEZA MFUMO WA NHIF WA KUJIHUDUMIA KUPITIA SIMU JANJA
WANANCHI WAPONGEZA MFUMO WA NHIF WA KUJIHUDUMIA KUPITIA SIMU JANJA
-Wasema unaongeza uwazi, ufanisi na kuokoa muda wa kupata huduma Na Grace Michael, Dar es Salaam WANANCHI na wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wamepongeza Mfumo wa Kujihudumia Binafsi (Self Service) unaowezesha wanachama kupata huduma mbalimbali kupitia simu janja, wakisema mfumo huo umeongeza uwazi katika utoaji wa huduma, kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kuokoa muda ambao awali walilazimika kuutumia kufika katika ofisi za NHIF. Wakizungumza kwa nyakati tofauti walipotembelea banda la NHIF katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, wananchi hao walisema maboresho ya mifumo ya kidijitali ya NHIF yameongeza ufanisi na kuimarisha usimamizi wa huduma za bima ya afya. Bw. Emmanuel Selemani alisema mfumo huo unampa mwanachama uwezo wa kuona historia ya huduma zote alizopata katika vituo vya kutolea huduma za afya, hatua inayochangia kuongeza uwazi na kuwapa wanachama nafasi ya kushir…