WANANCHI WAONYA DHIDI YA MAANDAMANO, WASISITIZA UMUHIMU WA AMANI NA UTULIVU
WANANCHI WAONYA DHIDI YA MAANDAMANO, WASISITIZA UMUHIMU WA AMANI NA UTULIVU
Baadhi ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wamewataka vijana kuepuka kushiriki kwenye maandamano yanayoweza kuvuruga amani na utulivu wa nchi, wakisema mazingira ya amani ndiyo msingi wa maisha ya kila siku, shughuli za kiuchumi na maendeleo ya wananchi. Akizungumza na chombo hiki cha habari leo Jumamosi Julai 04, 2026, Mkazi wa Magomeni Jijini Dar es Salaam, Bibi Neema Mkasi amesema vijana wanapaswa kuepuka kufuata mikumbo inayoweza kuwaingiza katika matatizo, akieleza kuwa watu wengi wenye kipato cha chini hawana akiba ya chakula wala fedha za kuwasaidia endapo kutatokea vurugu. "Mama Samia awe na amani, vijana tuwatake wasifuate mikumbo, wataumia na kuathirika, waache, wajipe muda wa kushughulika. Wengi tunaishi maisha ya chini, hatuna akiba yoyote ya chakula wala fedha, kwa hiyo vurugu zikitokea sisi wa hali ya chini kiuchumi ndio tutaathirika zaidi." amesema Bi. Mkasi. Kwa upande wake Bw. Madandi Donald, mjasiriamali wa Ilala Dar Es Salaam amesema kuwa amani ni nguzo muhi…