WANANCHI WAJIFUNZA KUTAMBUA UBORA NA THAMANI YA MADINI YA VITO
WANANCHI WAJIFUNZA KUTAMBUA UBORA NA THAMANI YA MADINI YA VITO 📍Dar es Salaam Wananchi wanaotembelea banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba) wanaendelea kunufaika na elimu kuhusu matumizi ya kifaa cha Gemmological Torch, kinachotumika kutambua ubora na thamani halisi ya madini ya vito. Akitoa elimu katika banda hilo, Mjiolojia na Mjimolojia Mwandamizi kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi-Mirerani, Selemani Khamisi, amesema thamani ya madini ya vito hupimwa kwa kuzingatia vigezo vinne vikuu vinavyojulikana kitaalam kama 4Cs, ambavyo ni rangi (Colour), uzito (Carat), ubora (Clarity) na umbo la ukataji (Cut). Amesema pamoja na matumizi ya Gemmological Torch, wataalam pia hutumia vifaa vingine vya kitaalam ikiwemo Head Loupe, Table Lamp na Price Guide ya Serikali ili kufanya tathmini ya kina ya ubora wa jiwe. Uchunguzi huo huwezesha kubaini nyufa, mipasuko, uchafu wa ndani (inclusions), pamoja na ubora na ukolezi wa rangi ya jiwe. “Kadiri jiwe linavyokuwa na rangi ang’avu, ubora mzuri wa ndani, uz…