WACHIMBAJI WADOGO WAISHUKURU SERIKALI KWA USAMBAZAJI WA UMEME MIGODINI

WACHIMBAJI WADOGO WAISHUKURU SERIKALI KWA USAMBAZAJI WA UMEME MIGODINI
▪️Zaidi ya Shilingi Bilioni 7 zatumika kusambaza umeme maeneo ya migodi ▪️Waziri Mavunde azindua mradi wa umeme katika Mgodi wa Igalula ▪️Akagua miradi ya maji na ujenzi wa shule za awali na msingi wilayani Nyang’hwale Nyang’hwale, Geita Wachimbaji wadogo wa madini wilayani Nyang’hwale, mkoani Geita, wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza katika upatikanaji wa nishati ya umeme kwenye maeneo ya migodi, hatua inayopunguza gharama za uzalishaji na kuongeza tija katika shughuli za uchimbaji. Shukrani hizo zimetolewa wakati Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, alipozindua mradi wa kuzalisha nishati ya umeme wenye uwezo wa KVA 500 kwenye Mgodi wa wachimbaji wadogo katika eneo la Igalula, wilayani Nyang’hwale. Mradi huo umetekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 426 na ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha miundombinu ya nishati katika maeneo ya uchimbaji wa madini. A…