VIONGOZI WA VIJIJI WAONYWA KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA ARDHI KIHOLELA
VIONGOZI WA VIJIJI WAONYWA KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA ARDHI KIHOLELA Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makakazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akiakabidhi hati za Hakimiliki za Kimila kwa wananchi wa Misungwi mkoani Mwanza wakati wa hafla ya kukabidhi hati hizo iliyofanyika wilayani humo Julai 6, 2026. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bi. Johari Simizi. Munir Shemweta, Misungwi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo amewatahadharisha viongozi wa vijiji nchini kuacha kujihusisha moja kwa moja na uuzaji wa ardhi bila kufuata taratibu za kisheria, akisema tabia hiyo imekuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini. Dkt. Akwilapo ametoa onyo hilo Julai 6, 2026 wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakati wa hafla ya kukabidhi hati 668 za hakimiliki za kimila kwa wananchi wa vijiji vya Ndinga na Lubuga. Alisisitiza kuwa viongozi wa vijiji, wakiwemo wenyeviti, ni wasimamizi wa ardhi na si wauzaji, hivyo maamuzi ya kuuza ardhi ya kijiji yanapaswa kufanywa kwa kufuata sheria kupitia mikutano ya vijij…