VIONGOZI NA WANANCHI WAHIMIZWA KUDUMISHA AMANI NA MSHIKAMANO KUPITIA UPENDO NA KUHESHIMU TOFAUTI
VIONGOZI NA WANANCHI WAHIMIZWA KUDUMISHA AMANI NA MSHIKAMANO KUPITIA UPENDO NA KUHESHIMU TOFAUTI
Home Licha ya uwepo wa tofauti za kiitikadi, dini na tamaduni katika jamii ya sasa, mafundisho ya viongozi wa kiroho na maandiko ya kidini yameendelea kusisitiza kuwa tofauti hizo zinapaswa kuwa fursa ya kuishi kwa heshima, upendo na mshikamano badala ya kuwa chanzo cha migawanyiko na uhasama. Akizungumzia misingi ya amani, maandiko mbalimbali na viongozi wa kimataifa wamekuwa wakikumbusha umuhimu wa binadamu kukubali kutofautiana kwao kama njia ya kujenga jamii imara. Mafundisho ya dini ya Kikristo yanataja amri ya kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda mwenyewe kama nguzo kuu ya mahusiano ya kibinadamu, wakati Uislamu kupitia Qurani Tukufu unasisitiza kuwa kuumbwa kwa wanadamu katika makabila na mataifa mbalimbali ni kwa ajili ya kufahamiana na kwamba thamani ya mtu hupimwa kwa maadili na uchaji Mungu badala ya rangi, kabila au dini yake. Aidha, viongozi wa kimataifa akiwemo Dalai Lama wamekuwa wakieleza kuwa upendo na huruma ni mahitaji ya msingi ya kuendeleza ubinadamu na sio anasa. Ms…