UTU WA TAIFA HUPIMWA KWA NAMNA LINAVYOWAJALI WAZEE WAKE – NAIBU WAZIRI MAHUNDI

UTU WA TAIFA HUPIMWA KWA NAMNA LINAVYOWAJALI WAZEE WAKE – NAIBU WAZIRI MAHUNDI
Na Jackline Minja WMJWM Bukoba, Kagera Serikali imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuhakikisha wazee nchini wanapata huduma bora na stahiki kwa kuimarisha makazi ya wazee, huduma za afya pamoja na mazingira salama yanayolinda utu na heshima yao. Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, alipofanya ziara ya kutembelea Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kiilima yaliyopo Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, kwa lengo la kujionea hali ya utoaji wa huduma, kusikiliza changamoto pamoja na kuhimiza maboresho ya ustawi wa wazee. Naibu Waziri Mahundi amesema Serikali itaendelea kuimarisha huduma za ustawi wa jamii kwa wazee ili kuhakikisha wanaishi katika mazingira salama, yenye heshima na yanayokidhi mahitaji yao ya msingi, ikiwemo huduma za afya, lishe, malazi na huduma za kijamii kwani Serikali inatambua mchango mkubwa wa wazee katika kujenga Taifa, hivyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuboresha huduma…