UJUZI WA VITENDO NI NGUZO YA KUJITEGEMEA KIUCHUMI - NAIBU WAZIRI MAHUNDI
UJUZI WA VITENDO NI NGUZO YA KUJITEGEMEA KIUCHUMI - NAIBU WAZIRI MAHUNDI
Na Jackline Minja, WMJJWM - Iringa Serikali itaendelea kuimarisha utoaji wa mafunzo ya ujuzi wa vitendo ili kuwawezesha wananchi, hususan vijana na wanawake, kujitegemea kiuchumi, kujiajiri na kuchangia maendeleo ya Taifa. Naibu Waziri Mahundi ameyasema hayo Julai 12, 2026 alipozungumza na wanafunzi wa mafunzo ya muda mfupi ya cherehani pamoja na watumishi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Kampasi ya Rungemba wilayani Mafinga , mkoani Iringa, ambapo amesema mafunzo hayo hayalengi kuwafundisha kushona nguo pekee bali kuwajengea uwezo wa kujitegemea, kuibua ubunifu na kutumia fursa zilizopo kuongeza kipato na kuboresha maisha yao. Amesema katika kipindi ambacho ajira rasmi zimekuwa na ushindani mkubwa, mafunzo ya ujuzi wa vitendo ni nyenzo muhimu ya kuwawezesha wananchi kujiajiri, kuanzisha biashara zao na hata kuajiri wengine, huku akiwataka wanafunzi hao kutumia maarifa waliopata kwa kuzingatia ubora wa kazi, ubunifu na mabadiliko ya teknolojia ili kuzalisha bidhaa zenye ushindani katika so…