Uchumi wa Buluu Ni Mlango Mpya wa Utajiri wa Taifa
Uchumi wa Buluu Ni Mlango Mpya wa Utajiri wa Taifa
Na Mwandishi Wetu UTEKELEZWAJI wa Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu umetajwa kuwa lango kuu la uchumi kutokana na fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta hiyo. Sekta ya uchumi wa buluu inahusisha mambo sita ambayo ni uvuvi, usafirishaji, utalii, gesi, petrol na umwagiliaji. Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uchumi wa Buluu na Uratibu Ofisi ya Makamu wa Rais, Magdalena Ngotolainyo, amesema hayo Juni 30, 2026 wakati akizungumzia uchumi wa buluu. Alisema Tanzania ni nchi iliyobarikiwa si kwa ardhi yenye rutuba pekee, wala si kwa madini, wanyamapori na vivutio vya utalii pekee, bali pia kwa utajiri mkubwa uliomo ndani ya maji yake. Bahari, maziwa, mito, mabwawa, maeneo oevu, maji chini ya ardhi na ukanda mpana wa pwani ni hazina ya kipekee ambayo, ikitumika kwa maarifa na uendelevu, inaweza kuwa injini mpya ya mageuzi ya kiuchumi na ustawi wa wananchi. Hii ndiyo nguvu ya Uchumi wa Buluu. Alisema uchumi wa buluu unahusisha matumizi endelevu ya rasilimali zinazopatikana katika bahari, maziwa…