UCHAGUZI CCM TANGA:MWANAFA AMPIGIA DEBE USTADH RAJAB
UCHAGUZI CCM TANGA:MWANAFA AMPIGIA DEBE USTADH RAJAB
📍Awaonya wajumbe wasifanye ushabiki wa Messi na Ronaldo Na Mashaka Mhando, Muheza. MBUNGE wa Jimbo la Muheza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma 'MwanaFA', amewataka wajumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo kutopepesa macho wala kubabaika linapokuja suala la kumchagua Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga katika uchaguzi mkuu wa chama hicho mwakani. MwanaFA ametoa kauli hiyo Leo Julai 23 wakati akizungumza na Wana-CCM wa kata za Kwakifua na Tingeni, ambapo ametumia jukwaa hilo kumpigia debe zito Mwenyekiti wa sasa wa mkoa huo, Ustadh Rajab Abdallah, akieleza kuwa rekodi ya kazi zake za kukijenga chama haijawahi kufikiwa na kiongozi yeyote nchini. Rekodi Zilizompa Kiki Ustadh Rajab Akijenga hoja ya kwanini wajumbe hawapaswi kufanya makosa, Mhe. Mwinjuma aliwataka wanachama hao kutaja mwenyekiti yeyote nchini aliyewahi kujenga nyumba za watumishi wa chama kila wilaya, ambapo wajumbe walijibu "hakuna." "Hebu nitajien…