TUME YA MADINI YAWAALIKA WAWEKEZAJI NA WANANCHI DITF KUJIONEA FURSA ZA SEKTA YA MADINI

TUME YA MADINI YAWAALIKA WAWEKEZAJI NA WANANCHI DITF KUJIONEA FURSA ZA SEKTA YA MADINI
Meneja mawasiliano na uhusiano wa Tume ya madini Greyson Mwase alievaa kifaa cha kisasa cha maabara cha X-Ray Fluorescence (XRF)kinachowezesha uchambuzi wa madini kwa haraka na kwa usahihi akiwa katika banda la Wizara ya madini katika maonesho ya 50 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam (DITF)akionesha namna kifaa hicho kilivyo na uwezo wa kufanya kazi kwa haraka  Baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la Wizara ya madini wakipima madini kwa kutumia kifaa cha kisasa cha maabara cha X-Ray Fluorescence (XRF) katika maonesho ya 50 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) Na Mwandishi wetu Malunde 1-Blog Dar es Salaam Tume ya madini imewaalika wawekezaji, wachimbaji wa madini, wadau wa sekta ya madini, wanafunzi na wananchi kutembelea banda la Wizara ya madini katika maonesho ya 50 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) ili kujionea fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya madini nchini. Kupitia banda hilo lililopo katika viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere, Tume …