TIRA YAZINDUA RASMI KIJIJI CHA BIMA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAONESHO YA SABASABA

TIRA YAZINDUA RASMI KIJIJI CHA BIMA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAONESHO YA SABASABA
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imezindua rasmi shughuli za Kijiji cha Bima katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam maaraufu kama maonyesho ya Sabasaba. Uzinduzi huo umeongozwa na Kamishna wa Bima, Dkt. Baghayo Saqware, na umehudhuriwa na viongozi wa kampuni za bima, madalali wa bima, watoa huduma na wadau mbalimbali wa sekta ya bima hapa nchini. Kijiji cha Bima ni jukwaa la kila mwaka linaloratibiwa na TIRA kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya bima kwa lengo la kuwasogezea wananchi elimu ya bima, ushauri wa kitaalamu na huduma mbalimbali za bima katika eneo moja. Kupitia jukwaa hilo, wananchi hupata fursa ya kujifunza umuhimu wa kuweka bima aina mbalimbali kwa lengo la kulinda maisha, afya, mali, biashara na uwekezaji wao kwa ujumla. Akizungumza katika uzinduzi huo, Dkt. Saqware, amesema kukua kwa sekta ya bima kunategemea sana uelewa wa wananchi kuhusiana na dhana nzima ya bima. Amesema jambo hilo linahitaji ushirikiano mkubwa wa wa…