TEA YAIMARISHA ELIMU YA AMALI KWA VIFAA VYA KISASA VYA USHONAJI
TEA YAIMARISHA ELIMU YA AMALI KWA VIFAA VYA KISASA VYA USHONAJI
Na Mwandishi Wetu WANAFUNZI wanaosoma mkondo wa elimu ya amali katika Shule ya Sekondari Dar es Salaam wameeleza kuwa ufadhili wa vifaa vya ushonaji uliotolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) umeleta mapinduzi makubwa katika utoaji wa mafunzo ya vitendo, hatua inayowajengea uwezo wa kujiajiri na kuanzisha biashara mara baada ya kuhitimu masomo yao. Akizungumza leo Julai 8, 2026 katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Mwanafunzi wa kidato cha tatu anayesoma fani ya ushonaji, Mariam Mitimingi, amesema alichagua mkondo wa amali baada ya kuona unatoa fursa kubwa za ajira na kujiajiri tofauti na kutegemea ajira rasmi pekee. Amesema kupitia mafunzo hayo, wanafunzi wanapata ujuzi wa kubuni na kushona mavazi mbalimbali huku wakiwa bado shuleni, jambo linalowawezesha kujijengea msingi imara wa taaluma na biashara za baadaye. "Nilichagua fani ya ushonaji kwa sababu niliona inanipa ujuzi wa moja kwa moja. Nikimaliza kidato cha nne nitakuwa tayari kuanzisha…