TBS YAKUTANA NA WADAU WA VIPODOZI, YASISITIZA VIWANGO NA USALAMA
TBS YAKUTANA NA WADAU WA VIPODOZI, YASISITIZA VIWANGO NA USALAMA
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limekutana na wadau wa sekta ya vipodozi nchini kwa lengo la kutoa elimu kuhusu matakwa ya viwango, ubora na usalama wa bidhaa hizo zinazotumika kwa kiasi kikubwa na Watanzania. Mkutano huo uliwakutanisha waagizaji, wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa vipodozi, pamoja na wadau wengine wanaohusika katika mnyororo wa bidhaa hizo, ukiwa na lengo la kuwajengea uelewa kuhusu taratibu na matakwa wanayopaswa kuzingatia ili kuhakikisha vipodozi vinavyofika kwa walaji ni salama na vyenye ubora. Akizungumza katika mkutano huo leo Julai 28, 2026 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, David Ndibalema, amesema shirika hilo limeitisha kikao hicho kwa kuzingatia jukumu lake la kisheria la kuthibitisha ubora na usalama wa bidhaa, ikiwemo vipodozi. Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Viwango, Sura ya 130, TBS ina wajibu wa kusimamia ubora na usalama wa bidhaa zinazoingia nchini na zinazozalishwa ndani ya nchi, hatua inayoleng…