TARURA YAIMARISHA UWEZO WA WAHANDISI KATIKA UJENZI WA MADARAJA NA MAKALAVATI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA 'WEHOLITE'
TARURA YAIMARISHA UWEZO WA WAHANDISI KATIKA UJENZI WA MADARAJA NA MAKALAVATI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA 'WEHOLITE'
-Yalenga kurejesha mawasiliano ya barabara kwa muda mfupi wakati wa dharura Dar es Salaam Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeendelea kuimarisha uwezo wa wataalamu wake kwa kuwapatia mafunzo ya matumizi ya teknolojia ya kisasa ya mabomba ya "Weholite" yanayotumika kujenga makalavati ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza ufanisi wa kurejesha mawasiliano ya barabara yanapokatika kutokana na mvua kubwa. Mafunzo hayo yamefanyika kwa ushirikiano na kampuni ya Mega Pipes Solutions Ltd na kuwashirikisha Mameneja wa TARURA kutoka mikoa yote 26 pamoja na wahandisi waliobobea katika usanifu wa madaraja. Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mhandisi Mshauri wa TARURA Makao Makuu, Pharles Ngeleja amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wahandisi na mameneja wa TARURA kutumia teknolojia ya "Weholite" katika kurejesha mawasiliano ya barabara kwa haraka hususan wakati wa mvua kubwa zinazosababisha kukatika kwa miundombinu. Amesema washiriki wamepatiwa el…