TANZANIA YANG’ARA CALC: BI. REHEMA KATUGA AIBUKA MWAKILISHI WA AFRIKA

Na Farida Mangube  Mtanzania Bi. Rehema Katuga kutoka Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria nchini (OCPD) ameibuka mshindi katika uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Uongozi na Usimamizi la Chama cha Wataalamu wa Uandishi wa Sheria wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Association of Legislative Counsel – CALC), na kuwa mmoja wa wawakilishi wawili wa Afrika katika baraza hilo. Baraza hilo, lenye wawakilishi wawili kutoka kila bara, lina jukumu la kusimamia na kufanya maamuzi muhimu kuhusu uendeshaji wa chama hicho cha kitaaluma kinachowakutanisha wataalamu wa uandishi wa sheria kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola. Bi. Katuga aliibuka mshindi katika uchaguzi uliowahusisha wagombea wanne kutoka Afrika, wakiwemo wagombea wawili kutoka Afrika Kusini, mmoja kutoka Namibia na yeye akiwa mwakilishi pekee kutoka Tanzania. Ushindi huo umeiwezesha Tanzania kupata nafasi ya uwakilishi katika chombo hicho muhimu cha kitaaluma. Akizungumzia umuhimu wa CALC, Bi. Katuga alisema chama hicho ni miongoni mwa …