TADB YAFIKIA HATUA MPYA YA UKUAJI: MTAJI WAFIKIA SHILINGI BILIONI 452.16
TADB YAFIKIA HATUA MPYA YA UKUAJI: MTAJI WAFIKIA SHILINGI BILIONI 452.16
Na Dotto Kwilasa, Dodoma Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, TADB, imeingia katika awamu mpya ya ukuaji baada ya mtaji wake kuongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka Shilingi bilioni 60 hadi kufikia Shilingi bilioni 452.16. Ongezeko hilo linaledwa na kuongezeka kwa uwekezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita katika sekta ya fedha za kilimo. Kwa mujibu wa uongozi wa benki hiyo, mtaji mpya umeipa TADB nguvu zaidi ya kutoa mikopo na kufadhili miradi inayolenga kubadilisha kilimo cha asili na kuwa kilimo cha kibiashara. Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Frank Nyabundege, amesema ongezeko la mtaji limekuja wakati sahihi ambapo nchi inahitaji kuongeza uzalishaji wa chakula na ajira kupitia kilimo. Amesema asilimia 73.6 ya jumla ya mikopo yote iliyotolewa na benki hiyo tangu kuanzishwa kwake, imetolewa katika kipindi cha miaka mitatu kati ya 2022 na 2025. Hii inaonyesha kasi ya utoaji wa huduma za kifedha imeongezeka mara tatu. “Kwa sasa tuna uwezo mkubwa zaidi wa kufikia wakulima wadogo, wafugaji na wavuv…