SERIKALI YAPONGEZA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA KWA UJENZI WA KARAKANA YA UZALISHAJI VIPURI

SERIKALI YAPONGEZA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA KWA UJENZI WA KARAKANA YA UZALISHAJI VIPURI
Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha SERIKALI imeipongeza Menejimenti na uongozi wa chuo cha ufundi Arusha (ATC), kutokana na bunifu mbalimbali zinazoendelea kufanywa chuoni hapo ikiwemo ujenzi wa karakana ya kisasa kwaajili ya kufundishia na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali. Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Hussein Mohamed Omar, 24Julai 2026 jijini Arusha katika ziara yake ya kikazi chuoni hapo. Dkt.Omar amesema ujenzi wa karakana hiyo ya kufundishia (Teaching Industry), utasaidia ongezeko kubwa la udahili wa wanafunzi chuoni hapo pamoja na kutoa fursa ya ajira kwa wanafunzi watakaopata elimu chuoni hapo. Amesema Menejimenti ya chuo hicho chini ya Mkuu wake wa chuo Profesa Mussa Chacha pamoja na uongozi wa bodi ya chuo unastahili kupongezwa kwa kuwa umekuwa ukitafsiri sera ya Elimu kwa vitendo. " Kwa niaba ya Serikali napenda kuwapongeza sana kuwekeza katika Ubunifu, lakini pia kwa kutafsiri sera ya Elimu kwa vitendo, ujenzi w…