SERIKALI KUZALISHA MAELF YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

NIRC: Arusha. Katika jitihada za kumkomboa mkulima mdogo kutokana na utegemezi wa mvua, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) inaendelea na mpango wa kuchimba visima 67,000 nchi nzima, mradi utakaozalisha maelfu ya ajira kwa vijana na kuleta uhakika wa chakula. Akiwasilisha mikakati hiyo katika Kongamano la 10 la Ununuzi wa Umma Mwaka 2026 jijini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Bw. Raymond Mndolwa, amebainisha kuwa mpango huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mara alipozindua mradi wa uchimbaji wa visima kwa wakulima wadogo katika maonesho ya kilimo Nanenane yaliyofanyika jijini Mbeya Mwaka 2023 Bw. Mndolwa ameeleza kuwa lengo kuu la mpango huo ni kuwawezesha wakulima wadogo kupata uhakika wa maji kwa ajili ya uzalishaji wa mwaka mzima. Amebainisha pia kuwa mradi huu unalenga kufikisha huduma za Umwagiliaji kwa makundi ambayo hayapo katika mfumo rasmi wa skimu za Umwagiliaji, hatua itakayoongeza uzalishaji, ajira na kipato cha wakulima na nchi kwa ujumla. “K…