SERIKALI KUIMARISHA UBORA WA HUDUMA ZA WAGONJWA MAHUTUTI KUPITIA MIONGOZO YA UTOAJI HUDUMA NA MAFUNZO KWA VITENDO
SERIKALI KUIMARISHA UBORA WA HUDUMA ZA WAGONJWA MAHUTUTI KUPITIA MIONGOZO YA UTOAJI HUDUMA NA MAFUNZO KWA VITENDO Na Cletus Sanga, WAF – Morogoro Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya Clinton Health Access Initiative (CHAI) imeendelea kuimarisha ubora wa huduma za wagonjwa mahututi nchini kwa kukamilisha kuandaa miongozo ya huduma za wagonjwa mahututi na mwongozo wa mafunzo kwa vitendo mahali pa kazi. Hayo yamesemwa Julai 23, 2026, mkoani Morogoro na Dkt. Michael Kiremeji, Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura na ajali kutoka Wizara ya Afya, wakati wa kikaokazi cha kuandaa miongozo ya idara ya wagonjwa mahututi( ICU), pamoja na mwongozo wa mafunzo kwa vitendo mahali pa kazi. “Tunaandaa miongozo hii ili kuhakikisha wataalamu wa afya wanatoa huduma zinazozingatia viwango vilivyowekwa, huku wakiendelea kuongeza ujuzi wakiwa kazini. Hii itaboresha ubora wa huduma na kuongeza usalama wa wagonjwa,” amesema Dkt. Kiremeji. Ameeleza kuwa mwongozo wa mafunzo kwa vitendo utasaidia kujenga mfumo endelevu wa kuwajengea uwezo wataalamu wa afya kupitia usimamizi wa karibu, ufuatiliaji wa ki…