SANGU: WALIOFUJA FEDHA ZA SHULE MFINGA WAFIKISHWE MAHAKAMANI
SANGU: WALIOFUJA FEDHA ZA SHULE MFINGA WAFIKISHWE MAHAKAMANI
Mbunge wa Jimbo la Kwela ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu akizungumza na Viongozi na Wananchi mara baada ya kukagua mradi wa Shule ya Msingi Mfinga iliyopo Sumbawanga, Mkoani Rukwa tarehe 19 Julai, 2026. ******************** Na: Mwandishi Wetu, Kwela Mbunge wa Jimbo la Kwela ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu ametaka watumishi wa umma wote wanaodaiwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za mradi wa ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mfinga kufikishwa mahakamani haraka baada ya kubainika kuwepo kwa viashiria vya matumizi mabaya ya fedha za umma. Akizungumza leo (Julai 19, 2026) baada ya kukagua mradi huo wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kuhamasisha shughuli za maendeleo katika Jimbo la Kwela, na kueleza kuwa hajaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo licha ya fedha nyingi zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wake. Ameele…