SADC YAHIMIZA MAGEUZI YA VIWANDA KWA MAENDELEO ENDELEVU YA UKANDA

SADC YAHIMIZA MAGEUZI YA VIWANDA KWA MAENDELEO ENDELEVU YA UKANDA
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Elias Magosi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Tisa ya Viwanda ya SADC (SADC Industrialisation Week 2026), inayoadhimishwa katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (ICC), jijini Durban, Afrika Kusini. Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo kujadili mikakati ya kuharakisha maendeleo ya viwanda na biashara ya kikanda. Washiriki wa Wiki ya Tisa ya Viwanda kutoka nchi wanachama wa SADC wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi, Katibu Mtendaji wa SADC, Elias Magosi, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (ICC), Durban, Afrika Kusini. Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Mahusiano wa Benki ya Maendeleo – TIB, Bw. Allan Chonjo akitoa maelezo kuhusu bidhaa na huduma zinazotolewa na Benki hiyo kwa baadhi ya wadau waliotembelea Banda la Tanzania, pembezoni mwa Mkutano wa Wiki ya Viwanda ya SADC (SADC Industrialisation Week 2026) unaofanyika k…