RC SHINYANGA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEO KISHAPU
RC SHINYANGA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEO KISHAPU Na Sumai Salum – Kishapu ARIDHISHWA NA HATUA YA MIRADI YA MAENDELEO KISHAPU Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, Julai 29, 2026 amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kishapu mkoani humo, ikiwa ni pamoja na mradi wa sekta za elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara, miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo pamoja na unufaishaji wa mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri. Akiwa katika ziara hiyo, Mhita amesema maendeleo yanayoonekana ni matokeo ya amani, utulivu na demokrasia ya kiuchumi inayowavutia wadau wa maendeleo na wawekezaji kushirikiana na Serikali kuboresha maisha ya wananchi. Mhita amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kujenga vyumba vya madarasa na kuboresha miundombinu ya shule ili kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya elimu katika mazingira bora, ikiwa ni pamoja na kuongeza uwiano wa madarasa na matundu ya vyoo kulingana na ida…