RC MTAKA AIPONGEZA WMA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA VIPIMO KWA WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA

RC MTAKA AIPONGEZA WMA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA VIPIMO KWA WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA
Njombe, Julai 30, 2026 Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, ameipongeza Wakala wa Vipimo (WMA) kwa kuendesha kampeni ya kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya vipimo kwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao.  Amesema kampeni hiyo itaimarisha biashara yenye haki, uwazi na uzingatiaji wa Sheria ya Vipimo, huku ikipunguza migogoro inayotokana na uelewa mdogo wa matumizi ya vipimo. Akizungumza ofisini kwake baada ya kupokea ujumbe wa WMA, Mtaka amesema elimu hiyo itasaidia kuondoa mkanganyiko unaojitokeza katika biashara ya mazao, hususani kuhusu matumizi ya lumbesa. Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakikamatwa kwa madai ya kubeba lumbesa kutokana na kutofahamu maana yake halisi. Alifafanua kuwa kujaza mzigo na kuweka kishungi juu yake hakumaanishi kuwa ni lumbesa. Aidha, amesema mzigo hutambulika kama lumbesa pale unapokuwa na uzito unaozidi kilo 100 hadi kilo 105. Amesema uelewa huu utawasaidia wafanyabiashara na wakulima kuzingatia sheria, kuepuka migogoro na kuongeza uamin…