RC MBONI MHITA AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM, 'RAIS SAMIA AMETOA TRILIONI 1.9 SHINYANGA'

RC MBONI MHITA AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM, 'RAIS SAMIA AMETOA TRILIONI 1.9 SHINYANGA'
Na Marco Maduhu, SHINYANGA Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa kipindi cha kuanzia Novemba, 2025 hadi Juni 2026. TAZAMA VIDEO πŸ‘‡πŸ‘‡ Amewasilisha taarifa hiyo leo kwa Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mabala Mlolwa. Mhita akisoma taarifa hiyo, amesema kwa kipindi cha uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wamepokea kiasi cha fedha sh. Trilioni 1.9 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo. Amesema, katika mapokezi ya fedha hizo wananchi wa Mkoa huo, wameshuhudia maendeleo ya haraka katika Nyanja za uzalishaji katika sekta ya kilimo, mifugo, madini, viwanda , biashara, pamoja na huduma za jamii, Afya, Elimu, Nishati na Maji. UTEUZI WA VIONGOZI Amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kumteuwa Mheshimiwa Patrobas Katambi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani na Mheshimiwa Salome Makamba kuwa Naibu Waziri wa Nishati. WASIFU WA MKOA Ames…