RC MAKALLA ATAKA WALIOLIPWA FIDIA KUONDOKA KUPISHA UJENZI WA BARABARA ZA AFCON
Na Happy Lazaro, Arusha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amewataka wananchi wote waliolipwa fidia kwenye maeneo zinapojengwa barabara zote kwaajili ya maandalizi ya Michuano ya Mpira wa Miguu Mataifa ya Afrika – AFCON 2027, kuondoka ili kuruhusu Mkandarasi kuendelea na utekelezaji wa miradi hiyo. Makalla ametoa agizo hilo leo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi na upanuzi wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa Km 9.1 kuanzia Makutano ya Ngarenaro – mzunguko wa Kisongo, Makutano ya Ngarenaro – Kona ya Nairobi na Makutano ya Ngarenaro – soko la Kilombero, kwa njia nne, mradi unaotekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 87.9. “Nimshukuru Mhe. Rais kwa kuwezesha ujenzi wa barabara hizi, niwaombe watalamu wasekta zote kutoa ushirikiano kuhakikisha hakuna kizuizi kwa Mkandarasi kufanya kazi, serikali ileshawalipa fidia wananchi wote kwa barabara zote za AFCON, zaidi ninawashukuru ambao wameshaondoka wameonesha uzalendo, na ambao hawajaondokaa niw…