RAIS WA MSUMBIJI KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU NCHINI TANZANIA

RAIS WA MSUMBIJI KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU NCHINI TANZANIA
Kufuatia mwaliko wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daniel Francisco Chapo Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini kuanzia tarehe 02 hadi 04 Julai, 2026.  Wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa Rais Chapo anatarajiwa kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.  Mazungumzo hayo yatajikita katika kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali zikiwemo biashara, uwekezaji, uchukuzi, nishati pamoja na kuangazia maeneo mapya ya ushirikiano yenye maslahi ya pamoja kwa wananchi wa nchi hizi mbili.  Mnamo tarehe 03 Julai 2026, Mheshimiwa Rais Chapo anatarajiwa kufungua rasmi Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama Sabasaba, yatakayowakutanisha wafanyabiashara, wawekezaji na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kukuza biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kiuchumi.  Aidha, Mheshimiwa Rais C…