Rais Samia: Mawasiliano Bora ya Serikali Ni Nguzo ya Uongozi na Maendeleo ya Taifa

Rais Samia: Mawasiliano Bora ya Serikali Ni Nguzo ya Uongozi na Maendeleo ya Taifa
Na Janeth Raphael - MichuziTv Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa mawasiliano ya Serikali yanapaswa kuwa ya kimkakati, yenye uratibu na yanayozingatia weledi ili kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali pamoja na kulinda maslahi ya Taifa. Rais Samia ametoa msisitizo huo leo Julai 28, 2026, wakati akifungua Semina Elekezi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu Umuhimu wa Mawasiliano Serikalini, iliyofanyika Ikulu ya Tunguu, Zanzibar. Semina hiyo ya siku mbili imewakutanisha kwa mara ya kwanza viongozi waandamizi kutoka Serikali zote mbili za Muungano kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu namna bora ya kuwasiliana na wananchi, kuhakikisha taarifa za Serikali zinatolewa kwa usahihi, kwa wakati na kwa lugha inayoeleweka. Akizungumza wakati wa ufunguzi, Rais Samia amesema mawasiliano si jambo la ziada katika utendaji wa Serikali, bali ni seh…