RAIS DKT. MWINYI: INDIA NI MSHIRIKA MUHIMU WA MAENDELEO YA ZANZIBAR
RAIS DKT. MWINYI: INDIA NI MSHIRIKA MUHIMU WA MAENDELEO YA ZANZIBAR NEW DELHI, INDIA, 19 JULAI 2026 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema uhusiano wa kihistoria baina ya Tanzania na India umeendelea kuimarika kupitia ushirikiano wa kisiasa, kidiplomasia, kiuchumi na kijamii, pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo imeleta mabadiliko chanya kwa wananchi. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 19 Julai 2026, alipokutana na Makamu wa Rais wa India, Mhe. C. P. Radhakrishnan, katika Afisi ya Makamu wa Rais wa India (Vice-President’s Enclave), jijini New Delhi. Rais Dkt. Mwinyi ameridhishwa na ukuaji wa biashara ya bidhaa baina ya Tanzania na India, ambayo imefikia dola za Marekani bilioni 9.02 katika mwaka wa fedha 2025/2026, kutoka dola bilioni 8.64 katika mwaka wa fedha 2024/2025. Aidha, India ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya uwekezaji nchini Tanzania, ambapo jumla ya uwekezaji wake umefikia takribani dola bilioni 4.08. Amesema ukuaji huo unaonesha kuwepo kwa fursa kubwa zaidi za kupanua bi…