POLISI NGARA WAWAFIKIA WATOTO YATIMA KUPITIA VITUO VYA MALEZI

POLISI NGARA WAWAFIKIA WATOTO YATIMA KUPITIA VITUO VYA MALEZI
Jeshi la Polisi Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera, limeendelea kuwafikia wananchi na makundi mbalimbali yenye uhitaji katika jamii kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na jamii, kutoa elimu pamoja na kuwajulia hali wananchi wanaolitegemea Jeshi hilo katika ulinzi wao na mali. Katika mwendelezo wa shughuli hizo, Jeshi la Polisi Wilaya ya Ngara limetembelea na kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika vituo vya kulelea watoto yatima Angel’s home pamoja na Kituo cha Kalkuta kilichopo Goyagoya, vinavyotoa huduma ya malezi kwa watoto yatima ambapo kituo hicho kina walea watoto kuanzia miaka 0 hadi 6. Akiongoza maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ngara, Mrakibu wa Polisi (SP) Machumu  Wang’uba amesema kuwa imekuwa ni utaratibu wa Jeshi la Polisi wilayani humo kuwafikia makundi yenye uhitaji kwa kuyapatia elimu mbalimbali pamoja na msaada wa mahitaji muhimu, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya Polisi na jamii. Aidha, (SP) Wang’uba ameiomba jamii kuendel…