OFISI YA WAZIRI MKUU NA TAASISI YA CHAKULA NA LISHE TANZANIA KUSHIRIKIANA KUANDAA MPANGO WA LISHE TAIFA

OFISI YA WAZIRI MKUU NA TAASISI YA CHAKULA NA LISHE TANZANIA KUSHIRIKIANA KUANDAA MPANGO WA LISHE TAIFA
Na Mwandishi Wetu- Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Bi. Debora Charwe amesema, Serikali ipo katika mchakato wa kuandaa Mpango wa Muda Mrefu wa Lishe wa Taifa (NN-LTP) ili kuongeza jitihada za sekta mtambuka katika kuboresha utekelezaji wa lishe kwa kipindi cha miaka 25 ijayo Bi. Debora ameyasema hayo leo tarehe 30 Juni, 2026 wakati akifungua Warsha ya mafunzo kuhusu kuandaa mpango wa muda mrefu wa lishe wa Taifa (National Nutrition Long Term Plan 2026-2050) ambayo inafanyika jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Juni 30 hadi Julai 02, 2026 Amesema, mafunzo hayo yanatolewa kwa Wataalam kutoka ngazi ya Wizara mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu uandaaji wa mipango ya muda mrefu wa lishe inayojumuisha sekta mtambuka pamoja na kubadilishana uzoefu kusaidia katika usanifu, muundo na taratibu za utekelezaji wa Mpango wa muda mrefu wa Lishe wa Taifa. Vilevile Bi. Debora amefafanua kuwa, mpango huo unaandaliwa chini ya usimamaizi wa Ofisi ya Waziri …