MWINYI: UCHUMI WA BULUU ULETE MANUFAA YA MOJA KWA MOJA KWA WANANCHI WA OACPS

MWINYI: UCHUMI WA BULUU ULETE MANUFAA YA MOJA KWA MOJA KWA WANANCHI WA OACPS
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS), Mhe. Moussa Saleh Batraki, pamoja na ujumbe wake, walipofika Ikulu Zanzibar, leo tarehe 23 Julai 2026. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS), Mhe. Moussa Saleh Batraki, pamoja na ujumbe wake, walipofika Ikulu Zanzibar, leo tarehe 23 Julai 2026. …………..  ZANZIBAR, 23 JULAI 2026 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameishauri Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) kuhakikisha maazimio na matamko yanayopitishwa katika mikutano yake yanatafsiriwa kuwa programu zinazotekelezeka na kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa nchi wanachama na wananchi wao Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 23 Julai 2026, alipokutana na…