MWENYEKITI WA UVCCM IRINGA APONGEZA MIRADI YA SERIKALI, ATAJA UWANJA WA NDEGE KUCHOCHEA AJIRA NA UCHUMI

MWENYEKITI WA UVCCM IRINGA APONGEZA MIRADI YA SERIKALI, ATAJA UWANJA WA NDEGE KUCHOCHEA AJIRA NA UCHUMI
NA DENIS MLOWE IRINGA  MWENYEKITI wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Aggrey Tonga, amesema vijana wa mkoa huo ni miongoni mwa wanufaika wakubwa wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, huku akiwataka wananchi kuendelea kuitunza na kuisimamia ili iendelee kuleta manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Aggrey alitoa kauli hiyo wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Iringa iliyotembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa jengo jipya la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Iringa. Alisema kamati hiyo imeshuhudia utekelezaji wa miradi katika sekta za elimu, afya, barabara, pamoja na miradi ya umwagiliaji na kilimo ambayo imeendelea kuboresha maisha ya wananchi. “Miradi yote tuliyoitembelea inaonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuwaletea wananchi maendeleo vijana ndiyo wanufaika wakubwa wa miradi hii kupitia ajira, biashara na fursa mbalimbali za kiuchumi,” alisema Aggrey. Akizungumzia mradi …