MKUU WA MKOA WA RUVUMA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA MBINGA KWA KUKUSANYA SHILINGI BILIONI 13.4 KATI YA LENGO LA KUKUSANYA SHILINGI BILIONI 10
Na Mwandishi Wetu, Mbinga MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Ahmed Abbas,ameipongeza Halmashauri ya Wilaya Mbinga kwa kupata hati safi kwa muda wa miaka kumi mfululilo huku Halmashauri hiyo ikifanikiwa kukusanya Sh.bilioni 13.4 kati ya lengo la kukusanya Sh.bilioni 10 hadi kufikia tarehe 30 Juni 2026. Abbas, ametoa pongezi hizo jana wakati akizungumza na watumishi na madiwani kwenye kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) na maagizo ya Kamati ya kudumu la Bunge hesabu za Serikali za mitaa(LAAC) “Mmeongeza Sh bilioni 3.4 hivyo mnastahili pongezi kubwa,nammshukuru Mheshimiwa Mbunge na Madiwani kwa namna mnavyoratibu vizuri Baraza linalopelekea kuwa na utulivu ukiacha changamoto chache ”alisema Rc Abbas. Aidha,amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Joseph Kashushura na menejimenti yake kuweka mpango bora wa matumizi ya ardhi,hata hivyo amewataka waendelee kusimamia vizuri ili ardhi iliyopo iweze kuwanufai…