MIXX Yajipanga Kutoa Huduma za Fedha na Mawasiliano maonesho ya Sabasaba
MIXX Yajipanga Kutoa Huduma za Fedha na Mawasiliano maonesho ya Sabasaba
Na Mwandishi Wetu AFISA Mtendaji Mkuu wa MIXX, Angelica Pesha, amesema kampuni hiyo imejipanga kikamilifu kuwahudumia wananchi wanaotembelea Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) kwa kuwapatia huduma mbalimbali za kifedha na mawasiliano kwa urahisi na usalama. Pesha alitoa kauli hiyo alipotembelea banda la MIXX katika maonesho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam. Alisema MIXX imeweka mazingira rafiki yatakayowawezesha wananchi kufanya miamala mbalimbali ya kifedha bila ulazima wa kubeba fedha taslimu, hatua ambayo inalenga kuongeza usalama na urahisi wa huduma kwa watumiaji. "Hatuna sababu ya wananchi kutembea na fedha taslimu wakati huduma zetu zinapatikana hapa bandarini. Tunawahimiza wote wanaotembelea Sabasaba kufika banda la MIXX ili wapate huduma za kifedha kwa haraka na kwa usalama," alisema Pesha. Aliongeza kuwa, pamoja na huduma za kifedha, MIXX pia inatoa huduma mbalimbali za mawasili…