MHE JOHARI: “KUFIKIA MALENGO DIRA 2050,TAIFA LINAHITAJI ZAIDI YA UTAALAMU WA SHERIA”
MHE JOHARI: “KUFIKIA MALENGO DIRA 2050,TAIFA LINAHITAJI ZAIDI YA UTAALAMU WA SHERIA” Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amefungua mafunzo ya tatu ya Bespoke kwa Mawakili wa Serikali, yalioandaliwa na kuratibiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambayo yameanza tarehe 15 Julai, 2026 na yatahimishwa tarehe 17 Julai, 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) Jijini Arusha. Mhe. Johari amewasisitiza Mawakili wa Serikali kuhakikisha wanasimamia vyema Utawala wa Sheria katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuishauri Serikali ipasavyo kuendelea kuzingatia sheria ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2050. *“Nitumie fursa hii kuwakumbusha washiriki wote kuwa, tunapoendelea katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2050 ni muhimu kufahamu kuwa, Taifa linahitaji zaidi ya utaalamu wetu wa sheria.”* Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Aidha, Mhe. Johari amewakumbusha Mawakili wa Serikali kutambua nafasi yao katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050, ambapo ameeleza kuwa utekelezaji wa malengo ya yake unategema kwa kiwango kikubwa uwezo wa Mawakili…