MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA KUIMARISHA UWAZI NA USHINDANI WA BIASHARA YA MIFUGO
MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA KUIMARISHA UWAZI NA USHINDANI WA BIASHARA YA MIFUGO Wafugaji nchini wanatarajiwa kunufaika na biashara ya kisasa ya mifugo baada ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) kuanza kuingiza mifugo katika Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, utakaounganisha taarifa za mifugo kidijitali na kuwawezesha wanunuzi kushindana kwa uwazi kupitia Soko la Bidhaa Tanzania (TMX). Akizungumza katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Bw. Asangye Bangu, amesema baada ya mafanikio ya kusimamia bidhaa 18 za mazao ya kilimo kupitia mfumo huo, sasa bodi imepanua huduma zake kwa kujumuisha mifugo. Amesema hatua hiyo inatokana na mahitaji ya wafugaji waliokuwa wakihoji kwa nini mfumo huo unawanufaisha wakulima pekee huku sekta ya mifugo ikibaki nje. “Tumekuja na bidhaa mpya ambazo zimeongezwa kwenye mfumo, na kubwa zaidi tumewafikia wafugaji. Tulikuwa tunasimamia bidhaa 18 za mazao ya kilimo, lakini sasa tumeingia rasmi kwenye bidhaa za mifugo,” amesema. Bw. Bangu amesema WRRB inalenga kuunganisha b…