MCT YAFANYA MKUTANO WA MASHAURIANO NA VIONGOZI WA SEKTA YA HABARI, YASISITIZA KUIMARISHWA KWA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MCT YAFANYA MKUTANO WA MASHAURIANO NA VIONGOZI WA SEKTA YA HABARI, YASISITIZA KUIMARISHWA KWA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura, akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Siku Mbili wa Mashauriano kati ya MCT na viongozi wa vyombo vya habari unaofanyika mkoani Morogoro Julai 16–17, 2026. Mkutano huo unajadili mafanikio, changamoto na mustakabali wa tasnia ya habari nchini katika kipindi cha miaka 30 ya mfumo wa kujisimamia. Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura, akifungua Mkutano wa Siku Mbili wa Mashauriano kati ya MCT na viongozi wa vyombo vya habari unaofanyika mkoani Morogoro Julai 16–17, 2026. Katibu Mtendaji wa MCT, Ernest Sungura (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa Siku Mbili wa Mashauriano kati ya MCT na viongozi wa vyombo vya habari unaofanyika Morogoro Julai 16–17, 2026. Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Baraza la Habari Tanzania (MCT) limeendelea kuwa nguzo muhimu katika kulinda uhuru wa vyombo vya habari, kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari na kusimamia maadili ya wanahaba…