Mbunge wa Ulanga Aomba Serikali Kujenga Barabara ya Lupiro–Mahenge

Mbunge wa Ulanga Aomba Serikali Kujenga Barabara ya Lupiro–Mahenge
Na Farida Mangube  Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Alaudin Hashim, ameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa kipande cha barabara ya Lupiro–Mahenge, akisema ni muhimu kwa usafirishaji wa mazao ya kilimo na madini katika Wilaya za Ulanga na Malinyi, Mkoa wa Morogoro. Ametoa ombi hilo wakati wa hafla ya kumkabidhi mkandarasi kazi ya ujenzi wa Daraja la Namuhanga lililopo Tarafa ya Lupiro. Daraja hilo lilisombwa na mafuriko, jambo lililosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wa Wilaya za Ulanga na Malinyi. Mbunge Salim amesema ana imani ujenzi wa daraja hilo utakamilika kwa wakati kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa mvua, ili kurahisisha shughuli za kiuchumi, hasa kilimo ambacho ndicho tegemeo kuu la wananchi wa maeneo hayo. «“Tunashukuru sana Serikali kwa kutuona sisi wananchi wa Wilaya za Ulanga na Malinyi. Wananchi sasa wanaenda kuondokana na adha iliyokuwa ikiwapata kutokana na kusombwa kwa Daraja la Namuhanga,” amesema Mbunge Salim.» Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesem…