MBUNGE WA KALENGA AKABIDHI MIFUKO 100 YA SARUJI, ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI MAGUNGA

MBUNGE WA KALENGA AKABIDHI MIFUKO 100 YA SARUJI, ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI MAGUNGA
NA DENIS MLOWE,IRINGA  MBUNGE wa Jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga, ameendelea kuunga mkono jitihada za maendeleo katika jimbo lake baada ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa nyumba ya watumishi katika Kijiji cha Magunga, Kata ya Maboga. Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Kiswaga alisema mchango huo ni sehemu ya juhudi zake za kuhakikisha mazingira bora ya kazi yanapatikana kwa watumishi wanaohudumu katika eneo hilo. Alisema tayari aliwahi kutoa bati 100 kwa ajili ya mradi huo na akaahidi kuendelea kushirikiana na wananchi hadi ujenzi utakapokamilika. Mwenyekiti wa Kijiji cha Magunga, Michael Mgimwa, alimpongeza Mbunge huyo kwa msaada alioutoa akieleza kuwa mifuko hiyo ya saruji itachochea kasi ya ujenzi wa nyumba hiyo Alisema lengo la wananchi ni kuukamilisha mradi huo ifikapo mwezi Oktoba ili kupunguza changamoto zinazowakabili baadhi ya watumishi wanaolazimika kupanga nyumba kutokana na uhaba wa makazi. Katika ziara hiyo, Mbunge Kiswaga pia alikuta…