MBUNGE MAGANGILA AKABIDHI MAGODORO KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WALIOWEKA KAMBI SHULE YA SEKONDARI IKINDA, AAHIDI KUWEKA UMEME WA JUA

MBUNGE MAGANGILA AKABIDHI MAGODORO KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WALIOWEKA KAMBI SHULE YA SEKONDARI IKINDA, AAHIDI KUWEKA UMEME WA JUA
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mhe. Mabula Magangila, amekabidhi magodoro kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Ikinda walioweka kambi shuleni kwa ajili ya maandalizi ya mitihani yao ya mwisho, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufaulu. Mhe. Magangila ametoa msaada huo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea hali ya wanafunzi hao waliokuwa wakilala katika mazingira yasiyoridhisha, jambo lililomgusa na kumfanya kuchukua hatua ya kuwapatia magodoro ili waweze kupata mapumziko bora na kuendelea na masomo yao kwa utulivu. Akizungumza wakati wa kukabidhi magodoro hayo, Mhe. Magangila amesema kuwa dhamira yake ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayeshindwa kufikia ndoto zake kutokana na changamoto za mazingira ya kujifunzia. "Nilipofika hapa na kuona hali ambayo watoto wetu wanapumzika, niliguswa sana. Elimu ni msingi wa maendeleo ya taifa letu, hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha wanafunzi wanapata ma…