MAWAZIRI AFRIKA WAKUBALIANA KUFANYA MAGEUZI YA KIUCHUMI, VIWANDA NA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA
MAWAZIRI AFRIKA WAKUBALIANA KUFANYA MAGEUZI YA KIUCHUMI, VIWANDA NA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA Naibu Waziri wa Fedha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiagana na Waziri wa Maliasili na Nishati wa Eswatini ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Mkutano wa 5 wa Kamati Maalum ya Mawaziri inayosimamia masuala ya Biashara, Utalii, Viwanda na Madini, Mhe. Prince Damian, baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa Pamoja wa 9 wa Kamati Maalum ya Mawaziri (STC) ya Umoja wa Afrika inayosimamia masuala ya Fedha, Uchumi, Mipango na Mtangamano pamoja na Mkutano wa 5 wa Kamati Maalum ya Mawaziri inayosimamia masuala ya Biashara, Utalii, Viwanda na Madini, jijini Abidjan, nchini Côte d’Ivoire. Na. Saidina Msangi, WF, Abidjan. Nchi za Afrika zimekubaliana kuweka kipaumbele katika ufadhili wa viwanda vinavyotegemea rasilimali za ndani ikiwemo madini na kuhakikisha kuwa zinaongeza thamani ya bidhaa na kuimarisha biashara ya ndani ya bara ili kujenga maendeleo jumuishi, endelevu na yenye tija. Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Serikali ya Jamhuri ya …