MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MKUTANO WA NNE WA URTHI WA HAYATI BENJAMIN MKAPA
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MKUTANO WA NNE WA URTHI WA HAYATI BENJAMIN MKAPA Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema unapotafakariwa mustakabali wa utoaji huduma za afya nchini, hakuna budi kutoa kipaumbele kwa vijana kama Hayati Benjamini Mkapa alivyoamini, ikiwemo kubuni programu zitakazowaandaa vijana kukabiliana na changamoto za siku zijazo kwa kujiamini. Makamu wa Rais amesema hayo, wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nne wa kuenzi na kuendeleza Urithi wa Hayati Benjamin William Mkapa na Maadhimisho ya Miaka 20 ya Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), uliyofanyika katika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Amesema Vijana ndiyo viongozi wa sekta ya afya wa kesho, watumishi wa afya na watafiti wajao. Makamu wa Rais amesema Maisha na uongozi wa Hayati Benjamin Mkapa unatoa mafunzo mengi hususani katika usimamizi na uendelezaji wa sekta ya afya nchini kwa kuwa alitambua nafasi ya afya bora…