MADEREVA WASISITIZWA USAFIRISHAJI SALAMA WA KEMIKALI
MADEREVA WASISITIZWA USAFIRISHAJI SALAMA WA KEMIKALI
Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kusini, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Hadija Mwema (aliyesimama) akizungumza na wawezeshaji pamoja na madereva wanaosafirisha makaa ya mawe, wakati akifungua mafunzo ya usafirishaji salama wa kemikali kwa madereva zaidi ya 90 mkoani Ruvuma. Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku mbili kuanzia Julai 23 hadi 24, 2026, wilayani Songea. Ruvuma. **************** Na Okello Thomas Madereva wanaosafirisha makaa ya mawe nchini wamehimizwa kuzingatia kikamilifu sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia usafirishaji wa kemikali na bidhaa hatarishi ili kulinda usalama wa wananchi, mazingira na mali, sambamba na kuhakikisha shughuli za usafirishaji zinafanyika kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa. Wito huo umetolewa leo na Meneja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kusini, Dkt. Hadija Mwema wakati akifungua mafunzo ya usafirishaji salama wa kemikali yaliyowahusisha madereva wa malori yanayosafirisha makaa yamawe wilaya ya Songea mkoani …