KUNENGE: MAOFISA MAENDELEO WAFUATE DIRA YA TAIFA 2050 KUACHA TABASAMU KWA WANANCHI
KUNENGE: MAOFISA MAENDELEO WAFUATE DIRA YA TAIFA 2050 KUACHA TABASAMU KWA WANANCHI Mwamvua Mwinyi,Kibaha Julai 30,2026 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa rai kwa maofisa maendeleo ya Jamii kuhakikisha wanazingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, akisisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuacha tabasamu kwa wananchi badala ya kujivunia ujenzi wa majengo pekee. Ametoa rai hiyo wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Maafisa Maendeleo ya Jamii kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Kibaha Julai 29,2026 kilichowakutanisha maofisa maendeleo ya Jamii, wakuu wa divisheni na vitengo, wakuu wa idara pamoja na viongozi wa taasisi za Serikali na binafsi. Kunenge alisema matarajio ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona viongozi wanaacha alama ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi, akisisitiza kuwa mafanikio ya Serikali hayapaswi kupimwa kwa idadi ya majengo yaliyojengwa bali kwa tabasamu la wananchi kutokana na huduma bora wanazopata. Kunenge alieleza Maofisa Maendeleo ya Jamii ni kiungo wanaozifahamu changamoto za wananchi katika maeneo yao, hivy…