KIONGOZI WA MWENGE ATAKA ELIMU YA UKIMWI ITOLEWE KWA VIJANA.

KIONGOZI WA MWENGE ATAKA ELIMU YA UKIMWI ITOLEWE KWA VIJANA.
Na John Walter -BABATI Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU), hususan kwa vijana wa rika balehe, akieleza kuwa ugonjwa huo bado upo na unahitaji tahadhari pamoja na mabadiliko ya tabia. Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa afua za UKIMWI katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara iliyopo mtaa wa Miomboni, Halmashauri ya Mji wa Babati, Mwang’onda amesema ni muhimu kuendelea kuandaa makongamano na kampeni za kuhamasisha wananchi kujitokeza kupima VVU, kupata ushauri nasaha na kufahamu hali zao za afya. Amesema watumishi wa afya na wadau wanaotekeleza afua za UKIMWI wanafanya kazi ya kitume waliyopewa na Mwenyezi Mungu ya kuokoa maisha ya watu, hivyo wanapaswa kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa uadilifu na kujituma katika kuwasaidia wengine. “UKIMWI bado upo. Vijana, hasa wa rika balehe, wanapaswa kuwa makini na kuendelea kupewa elimu sahihi ili kujik…